Friday, March 22, 2019

HISTORIA YA KOMPYUTA (1642) (COMPUTER GENERATION)

 
Msomi mmoja kutoka Ufaransa aliyekuwa anaitwa Pascal, alianzisha chombo cha kufanyia hesabu, ambacho alikitengeneza kwa ajili ya kumsaidia baba yake katika kazi za hesabu, lakini hakikuwa na sifa bora kama ilivyotakiwa. Kisha baada ya hapo kiliendelezwa na msomi mwengine kutoka Ujerumani, ambaye alijulikana kwa jina la Lebnitz na kuzidishwa ubora zaidi, kikawa kinafanya kazi zote za hesabu, kama vile kujumlisha, kutoa, kugawanya na kuzidisha, badala ya kufanya kazi za kuzidisha na kugawanya tu. Kisha msomi mwengine kutoka Uingereza alikuja kuanzisha chombo chengine cha hesabu, ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu. Chombo hicho kilikuwa na sehemu kuu tatu, ambazo sehemu ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu, sehemu ya pili ilikuwa ni kwa ajili ya kufanyia hesabu, na sehemu ya tatu na ya mwisho ilikuwa ni kwa ajili ya kuchapishia. Pascaline first Calculator


HATUA YA MWANZO (1944)

Kipindi cha mwaka 1944 kinajulikana kuwa ni mwanzo wa kudhihiri kompyuta. Kompyuta katika kipindi hicho ilikuwa ina sura tofauti na hivi sasa, kwani ilikuwa ni kubwa mfano wa chumba, na ilikuwa inatumika kwa ajili ya kufanyia hesabu tu, na ilikuwa inajulikana kwa jina la (ENIAC) Electronic Numerical and Calculation. Na mwisho wa mwaka 1951 ilianzishwa kompyuta nyingine ambayo ilikuwa inaitwa Unifac, na ilitengenezwa kwa ajili ya kufanyia biashara, na ilikuwa ni chombo pekee ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu.

HATUA YA PILI (1958)

Kipindi cha mwaka 1958 kilifanikiwa kuendeleza chombo cha kompyuta, ambapo kilianzishwa chombo kinachoitwa Transistor, ambacho kiliwezesha kutengeneza kompyuta yenye umbo dogo baada ya kuwa na umbo kubwa mfano wa chumba. Vile vile chombo cha Transistor kiliwasaidia watumiaji wa kompyuta kipindi hicho kuepukana na joto kali lililokuwa linatoka kwenye kompyuta hiyo na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Na mwanzo wa miaka ya sitini shirika la IBM lilianzisha chombo chengine cha kompyuta ambacho kilikuwa na maendeleo zaidi katika kipindi hicho.

HATUA YA TATU (1964)

Kipindi hichi kilileta maendeleo makubwa sana katika kompyuta, ambapo chombo cha kompyuta kilitengenezwa kwa kutumia (Integrated Circuits) chombo hicho kilichukua nafasi ya Transistor. Na pamoja na maendeleo makubwa kutokea mwaka 1972 shirika la Intel lilifanikiwa kutengeneza Processor ndogo ambayo ilibadilisha sura nzima ya kompyuta katika umbo dogo sana (Mini Computer). Na hiyo ilikuwa ni sifa pekee ya mabadiliko makubwa ya kompyuta, na katika kipindi cha mwaka 1975 shirika la IBM lilianzisha kompyuta ya kutumiya mtu mmoja (Personal Computer), vile vile katika kipindi hicho zilianzishwa programu za kuendeshea vifaa vya kompyuta, na miongoni mwa programu hizo ilikuwepo programu ya (Dos) Disk Operating System, Application Programs, na programu za kutengeneza picha (Graphics).




HATUA BAADA YA HATUA YA NNE (1995)

Kitu kinachosifika sana katika kipindi hichi ni kudhihiri kwa programu za Windozi na kuwa kama ni mazingira pekee ya kuendeshea kompyuta, na inajulikana wazi kwamba windozi ni kiini cha uendeshaji katika kazi za kompyuta, na imeitwa windozi kwa sababu unaweza kuitumia kufanyia kazi nyingi kwa wakati mmoja kwenye madilisha tofauti, kwa mfano pale mtumiaji anapokuwa anasubiri windozi moja ifunguke anaweza kuwa anasoma au kufanya kazi nyingine kwenye windozi nyingine pia.. Na windozi ya kwanza kudhihiri ilikuwa ni Windows 95, 98, 2000, Millennium kisha Windows XP, vili vile zilianzishwa programu maalumu kutoka kwenye shirika la Microsoft, kama vile Microsoft Office 97, Microsoft Office 2000 na Microsoft Office 2003, ambazo ambazo zinakusanya ndani yake Microsoft Word, Excel, Access na Power Point, pia zinajulikana kwa jina la application programs. Kisha kiliendelezwa kifaa cha Processor kutoka Pentium kwenda Pentium 2, Pentium 3 na Pentium 4, pamoja na kuzidi uwepesi wa kufikia vitu mpaka Giga Byte 2. Pia ilizidishwa nafasi ya kuhifadhia data ndani ya Hard disk kiasi cha kufikia Giga Byte 300, na kufikia nafasi ya Ram zaidi ya Mega Byte 512







1 comment:

Maintain your PC

         COMPUTER MAINTENANCE                                    Computer maintenance is the practice of keeping computers in a goo...